Magazeti ya Alhamisi, Machi 5, yameangazia barua ya kivita ambayo Rais Uhuru Kenyatta aliandikia serikali ya Somalia kulaani shambulio la Jumatatu, Machi 2 katika eneo la Mandera kutoka kwa wanajeshi wa Mogadishu.
Magazeti haya pia yanaripoti kuhusu mikakati ambayo serikali imeweka ili kuzuia kusambaa kwa homa hatari ya China ya corona kuingia Kenya.
Habari Nyingine: Bingwa wa Olimpiki Mkenya Ruth Jebet, apigwa marufuku miaka 4 kwa kutumia pufya
Habari Nyingine: Hofu yatanda katika Gereza la Embu baada ya wafungwa 27 kuambukizwa TB
1. People Daily
Gazeti hili linaripoti kuhusu ripoti ya visa vya mauaji ya kiholela na kupotea kwa watu ambayo iliwasilishwa bungeni.
Ripoti hiyo ilifichua kwamba kuanzia Oktoba 2018 hadi Februari 2020, yamkini visa 210 ya mauaji yaliyosababishwa na polisi yaliripotiwa huku maeneo ya mabanda yakiathirika zaidi kwa sababu ya ukosefu wa ajira.
Ripoti hiyo ilisema Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo na Mto wa Ol Donyo Sabuk ndio maeneo ambayo miili ya waathiriwa ilikuwa ikitupwa baada ya kuteswa na kisha kumiminiwa risasi na polisi.
Jijini Nairobi, ripoti hiyo iliorodhesha maeneo ya Dandora, Huruma, Mathare, Pangani, Kariobangi, Mukuru Kwa Njenga na Kamukunji kama maeneo ambayo washukiwa wanaweza kuawa kutokana na mienendo ya polisi.
Stesheni zingine ni pamoja na Kituo cha Polisi cha Nyeri ya Kati, Eldoret ya Kati na and Stesheni ya Polisi ya Nyali ya Kati.
2. Taifa Leo
Viongozi wa kidini kutoka eneo la Nyanza wamemkashifu vikali Naibu wa Rais William Ruto kwa mazoea yake ya kumtambua kiongozi wa ODM Raila Odinga kama mganga.
Mwenyekiti wa viongozi wa kidini katika eneo hilo Washington Ngoyo alimwambia Ruto kuwa Raila ni Mkristo mcha Mungu ambaye alibatizwa na hana nguvu za giza.
Matamshi ya Ngoyo yalikaririwa na naibu wake Julius Otieno ambaye alimshauri Ruto kusoma kitabu cha Matayo 7.21 kinachosema “Si kila mtu aniitaye bwana ataingia kwenye ufalme wa mbinguni, ila afanyaye mapenzi ya babangu aliye mbinguni.”
Viongozi hao wamemuhimiza Ruto kuunga maridhiano kati ya Rais na Raila endapo anamtaka waziri mkuu wa zamani kuunga mkono azma yake ya kuingia Ikulu 2022.
3. The Star
Gazeti la The Star linaripoti kuhusu visa vya mimba ya mapema ambavyo vinaendelea kuwa kidonda sugu kwenye sekta ya Elimu na vita dhidi ya Ukimwi.
Utafiti mpya umetambua kuwa kaunti ya Nairobi ndio inaongoza katika visa vya mimba ya mapema huku takriban wasichana 2,432 wachanga wakijifungua mwaka 2019.
Nakuru ni ya pili na visa 1,748, Kajiado (1,523), Kericho (1,006), Homa Bay (957), Narok (910), Garissa (901), Kisii (723), Bungoma (592), Turkana (560) na Kakamega (536).
Kaunti zenye idadi ndogo ya visa hivyo mnamo mwaka jana ni Isiolo (14), Lamu (22), Embu (25), Nyandarua (47), Kirinyaga (58), Elgeyo Marakwet (59).
Katika takwimu ya kitaifa jumla ya wasichana 379,573 wachanga walipachikwa mimba 2019.
4. The Standard
Duru katika chama cha ODM zinadai kwamba chama hicho kinatazamia kuwapokea wanachama wengi ambao waligura chamani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2017.
Kulingana nao, hii ni miongoni mwa mikakati ya kiongozi wa chama hicho Raila Odinga kuimarisha chama chake kwa maandalizi ya chaguzi za 2022 baada ya uongozi wa miaka 10 ya Rais Uhuru kutamatika.
Mnamo Jumatano, Raila aliwapokea wanachama wa zamani Jakoyo Midiwo, Teuben Ndolo, George Omondi, Oyugi Magwanga na Elizabeth Ongoro.
Raila hajatangaza bayana azma yake ya kuwania urais mwaka 2022 lakini sehemu ya wandani wake wana imani kuwa ataongoza chama hicho katika chaguzi za 2022.
5. Daily Nation
Wandani wa Naibu Rais William Ruto wanamtaka Uhuru kuongoza kampeni za Maridhiano (BBI) ili Ruto aweze kutoa maoni yake.
Wakingozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Caleb Kositany, viongozi hao wanamtaka Uhuru kuhudhuria mkutano wa BBI utakaoandaliwa Nakuru siku ya Jumamosi, Machi 21 na kuzima umaarufu wa Raila.
Kositany anasema Raila ni mgeni katika Chama cha Jubilee na hivyo hana mamlaka ya kupokea maoni ya BBI.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaYFyhJRmpJqfka%2BytbWMsphmoqWirrWtzahkppmTnbZugYyrrK2nXZa8r8XWmmSnmV2rtrC6xqixomWnlnqstcOipaJlm6q6trXTmmSrmZmhrm65xpqloJlencGuuA%3D%3D